MRADI WA MAENDELEO YA VIKUNDI VYA KIUCHUMI
Mradi wa Maendeleo ya Biashara ndogondogo unahusisha wafanyabiashara ndogondogo waliojiunga katika vikundi vya kiuchumi kwa lengo la kuchanga ujuzi wao ili wafanye kazi pamoja kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kazi zao pamoja na vikundi ambavyo wafanyabiashara ndogondogo hulenga kuhifadhi pesa kwa pamoja, Kukopeshana na Kuongeza mtaji.
UFUPISHO WA TAARIFA MUHIMU ZA MRADI
HUDUMA ZA MRADI | AINA YA VIKUNDI LENGWA | MAKUNDI YA WALEZI WA VIKUNDI |
Kufundishwa Kuhusu Uongozi na Usimamizi wa Vikundi na ukuwaji wa vikundi mpaka kuwa Kampuni | Vikundi vya Wafanyabiashara ndogo ndogo wanaofanya biashara pamoja | Halmashauri |
Kufundishana Mbinu za Kukuza Biashara na kupanua wigo wa Biashara | Vikundi vilivyoanzishwa na Taasisi za Fedha na kuvikopesha | Taasisi za Fedha |
Kufundishwa Usimamizi wa Fedha mambo ya mikopo, kuweka na Kusimamia malengo | Vikundi vilivyoanzishwa na mashirika mbalimbali | Mashirika Mabalimbali |
Kujumuisha watu wote walio katika vikundi katika kundi la Mtandaoni la Maendeleo ya Vikundi vya Kiuchumi kwa lengo la kubadilishana maarifa | Vikundi vilivyo anzishwa kutokana na Miradi ya mashirika ya kimataifa | Wadau wa Mashirika ya Kimataifa |
Kukutanisha vikundi, Mamlaka na Wadau mbalimbali kwa njia ya mtandao na mikutano mbali mbali | Vikundi Vilivyoanzishwa na Nyumba za Kulelea waraibu pamoja na DCEA | Nyumba za Kulelea Waraibu |
Bodi ya Usimamizi wa Malengo, Bajeti na Utawala bora | Vikundi vya kukopeshana na Viccoba vidogo | Taasisi za fedha, BOT, n.k |