Kuelekea uzinduzi wa Jukwaa la Biashara na Huduma (JBH), lililoanzishwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, lengo kuu ikiwa ni kuifanya Kariakoo kuwa kitovu cha biashara ndani ya Tanzania, Ukanda wa Afrika Mashariki (EAC), na Afrika ya Kusini na Kati (SADC). Jukwaa hili litawakutanisha wafanyabiashara wa EAC na SADC, watoa huduma, viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazouzwa Kariakoo, na mamlaka za serikali zinazoratibu biashara nchini.

Uzinduzi utafanyika tarehe 10 Oktoba 2024, ukifuatiwa na Mkutano wa Kilele kuanzia tarehe 21-23 Novemba 2024, ambao utawakutanisha wadau wote ili kuelezea muundo wa soko la kariakoo, kujadili fursa za Kariakoo, kutangaza bidhaa na huduma zinazopatikana kariakoo, na kuboresha uhusiano kati ya wafanyabiashara, wateja wao na viwanda. Wafanya biashara watapata nafasi ya kutangaza bidhaa zao, kujifunza mbinu mpya, na kuunganishwa na masoko mapya.

Kupitia jukwaa hili, wafanyabiashara watapata fursa ya kueleza changamoto zao, kupata taarifa stahiki, uzinduzi wa mafunzo, na msaada wa kutatua masuala muhimu kutoka kwa wataalamu na mamlaka za umma. Pia, litachangia katika kurahisisha taratibu za upatikanaji wa huduma na kuboresha mazingira ya biashara kwa kuwa na kliniki ya biashara.

Kwa maandalizi bora, Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na wadau wengine tunakuomba ujaze dodoso hili, ili kujenga uelewa wa pamoja na kuboresha taarifa na huduma zinazowalenga wafanyabiashara wa Kariakoo. Majibu yako yatatumiwa na wataalamu wa mamlaka kushauri watunga sera, kuandaa mafunzo na majibu yatakayoweza kuboresha biashara Kariakoo na kote nchini.

Tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa namba +255 775 731 306 / +255 754 731 306 au barua pepe biasharanahuduma@gmail.com endapo utahitaji maelezo zaidi. Vilevile, unaweza kuwasiliana na Bw. Peter Mbilinyi, Katibu wa JWK na Mratibu Mwenza, kupitia namba +255 718 382 021 au barua pepe info@jwk.or.tz.